Uteuzi wa Kidato cha Kwanza uwe wa haki

Man and Woman jumping off a cliff into a river

Jamaa wakionyesha mbwembwe kwa kujirusha kwenye mto  GNU Free Documentation License, Version 1.2

Imepakiwa - Thursday, October 30  2008  at 14:13

Kwa Mukhtasari

http://syndication.nation.co.ke

 

http://syndication.nation.co.ke

WALIMU Wakuu wa shule za upili, hasa za ngazi ya taifa, wanakutana leo (Ijumaa), kuanza kuwateua wanafunzi
watakaojiunga na kidato cha kwanza.
Uteuzi huo umeibua hisia kali, hasa kutoka kwa wadau katika sekta ya shule za kibinafsi.
Mwenyekiti wa chama cha Shule za Kibinafsi Bw John Mwai, ametishia kwenda mahakamani iwapo Serikali itaendelea na
mpango wa kuteua mwanafunzi mmoja kutoka shule za kibinafsi kwa kila watatu kutoka za umma.
Huenda shule za kibinafsi zikawa na hoja katika jambo hili. Watoto waliosoma katika shule za kibinafsi, bado ni
watoto wa Kenya. Kama walipata alama za kuwawezesha kujiunga na shule za kitaifa, hakuna sababu ya kuwanyima.
Lakini pia Bw Mwai na wenzake wanafaa kujiuliza; ikiwa mwanafunzi aliyesoma akiwa anakalia mawe atapata alama 380
na aliyekuwa akibebwa kwa gari, akisoma kwenye shule yenye vifaa vyote atapata alama 390, ni yupi anayestahili
nafasi katika shule ya kitaifa?
Katiba yetu inasema elimu ni haki ya kila mtoto bila kubaguliwa. Kwa hivyo, mtoto wa maskini aliyesoma katika shule
ya umma, akinyimwa nafasi hiyo, hawezi kwenda kupata nafasi katika shule nzuri ya upili ya kibinafsi.
Nayo Serikali kwa upande wake, inapaswa kuhakikisha kuwa inakamilisha pesa ilizoahidi kuzipa shule zilizopandishwa
ngazi majuzi.
Hakutakuwa na usawa kama mwanafunzi mmoja aliyepata alama 400 ataitwa kujiunga na Alliance au Mangu na mwenzake
aliyepata alama sawa na hizo ajiunge na Pangani, Maranda au Shimo La Tewa, ikiwa shule hizi hazitapewa vifaa vinavyohitajika kufaulisha masomo.Bila shaka, mwanafunzi aliye shule za kitaifa za kundi la kwanza atakuwa amemzidi mwenzake.
Shule za ngazi ya mkoa na wilaya pia zinafaa kufadhiliwa na Serikali ili viwango vya elimu viimarike katika shule
za umma.

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel